Ukristo
nyuma

Mithali 5

1Mwanangu, sikiliza kwa makini hekima yangu, sikiliza vizuri maneno yangu ya busara,

2ili uweze kutunza busara na midomo yako ihifadhi maarifa.

3Kwa maana midomo ya mwanamke kahaba hudondoza asali, na maneno ya kinywa chake ni laini kuliko mafuta;

4lakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo, mkali kama upanga ukatao kuwili.

5Miguu yake hushuka kuelekea kwenye kifo; hatua zake huelekea moja kwa moja kaburini.

6Yeye hafikiri juu ya njia ya uzima; njia zake zimepotoka, lakini yeye hajui.

7Sasa basi wanangu, nisikilizeni; msiache ninalowaambia.

8Njia zenu ziwe mbali naye, msiende karibu na mlango wa nyumba yake,

9usije ukatoa nguvu zako nzuri kwa wengine na miaka yako kwa aliye mkatili,

10wageni wasije wakasherehekea utajiri wako na jitihada yako ikatajirisha nyumba ya mwanaume mwingine.

11Mwishoni mwa maisha yako utalia kwa uchungu, wakati nyama na mwili wako vimechakaa.

12Utasema, “Tazama jinsi gani nilivyochukia adhabu! Tazama jinsi moyo wangu ulivyodharau maonyo!

13Sikuwatii walimu wangu wala kuwasikiliza wakufunzi wangu.

14Nimefika ukingoni mwa maangamizi kabisa katikati ya kusanyiko lote.”

15Kunywa maji kutoka kwenye kisima chako mwenyewe, maji yanayotiririka kutoka kwenye kisima chako mwenyewe.

16Je, chemchemi zako zifurike katika barabara za mji na vijito vyako vya maji viwanjani?

17Na viwe vyako mwenyewe, kamwe visishirikishwe wageni.

18Chemchemi yako na ibarikiwe na umfurahie mke wa ujana wako.

19Kulungu jike apendaye, kulungu mzuri: matiti yake na yakutosheleze siku zote, nawe utekwe daima na upendo wake.

20Kwa nini mwanangu, utekwe na mwanamke kahaba? Kwa nini ukumbatie kifua cha mke wa mwanaume mwingine?

21Kwa maana njia za mtu ni wazi kabisa mbele za Bwana, naye huyapima mapito yake yote.

22Matendo mabaya ya mtu mwovu humnasa yeye mwenyewe; kamba za dhambi yake humkamata kwa nguvu.

23Atakufa kwa kukosa nidhamu, akipotoshwa kwa upumbavu wake mwenyewe.

chanzo: Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

WEBREATH · 11:11

«He himself gives everyone life and breath and everything else» — Acts 17:25

Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.

WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath