Ayubu 17
1Moyo wangu umevunjika, siku zangu zimefupishwa, kaburi linaningojea.
2Hakika wenye mizaha wamenizunguka; macho yangu yamebaki kutazama uadui wao.
3“Ee Mungu, nipe dhamana unayodai. Ni nani mwingine atakayeweka dhamana kwa ajili yangu?
4Umezifunga akili zao zisipate ufahamu, kwa hiyo hutawaacha wapate ushindi.
5Kama mtu akiwashutumu rafiki zake ili apate ujira, macho ya watoto wake yatashindwa kuona.
6“Mungu amenifanya kitu cha dhihaka kwa kila mtu, mtu ambaye watu humtemea mate usoni.
7Macho yangu yamefifia kwa ajili ya majonzi; umbile langu lote ni kama kivuli.
8Watu wanyofu wanatishwa na hili; watu wasio na hatia wanasimama dhidi ya wasiomcha Mungu.
9Hata hivyo, waadilifu watazishika njia zao, nao wale wenye mikono safi wataendelea kupata nguvu.
10“Lakini ninyi njooni, ninyi nyote, jaribuni tena! Sitampata mtu mwenye hekima miongoni mwenu.
11Siku zangu zimepita, mipango yangu imevunjika, vivyo hivyo shauku za moyo wangu.
12Watu hawa hufanya usiku kuwa mchana, kwenye giza wao husema, ‘Mwanga u karibu.’
13Kama nyumba pekee ninayoitarajia ni kaburi, kama nikikitandika kitanda changu gizani,
14kama nikiuambia uharibifu, ‘Wewe u baba yangu,’ na kuliambia buu, ‘Wewe u mama yangu’ au ‘Dada yangu,’
15liko wapi basi tarajio langu? Ni nani awezaye kuona tarajio lolote kwa ajili yangu?
16Je, litashuka chini hadi kwenye malango ya mauti? Je, tutashuka pamoja mavumbini?”
WEBREATH · 11:11
«He himself gives everyone life and breath and everything else» — Acts 17:25
Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.
WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath