Ukristo
nyuma

Mwanzo 10

1Hawa ndio wazao wa Noa: Shemu, Hamu na Yafethi, ambao walizaa wana baada ya gharika.

2Wana wa Yafethi walikuwa: Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.

3Wana wa Gomeri walikuwa: Ashkenazi, Rifathi na Togarma.

4Wana wa Yavani walikuwa: Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu.

5(Kutokana na hawa mataifa ya Pwani yalienea katika nchi zao, kwa koo zao katika mataifa yao, kila moja kwa lugha yake.)

6Wana wa Hamu walikuwa: Kushi, Misraimu, Putu na Kanaani.

7Wana wa Kushi walikuwa: Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa: Sheba na Dedani.

8Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa duniani.

9Alikuwa mwindaji hodari mbele za Bwana. Ndiyo sababu watu husema, “Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda mbele za Bwana.”

10Vituo vyake vya kwanza katika ufalme wake vilikuwa Babeli, Ereki, Akadi na Kalne katika Shinari.

11Kutoka nchi ile alikwenda Ashuru, ambako alijenga Ninawi, Rehoboth-iri, Kala,

12na Reseni, iliyo kati ya Ninawi na Kala; huo ndio mji mkubwa.

13Misraimu alikuwa baba wa: Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi,

14Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti), na Wakaftori.

15Kanaani alikuwa baba wa: Sidoni mzaliwa wake wa kwanza, Hethi,

16Wayebusi, Waamori, Wagirgashi,

17Wahivi, Waariki, Wasini,

18Waarvadi, Wasemari na Wahamathi. Baadaye koo za Wakanaani zilitawanyika,

19na mipaka ya Kanaani ilienea kutoka Sidoni kuelekea Gerari hadi Gaza, kisha kuelekea Sodoma, Gomora, Adma na Seboimu, hadi kufikia Lasha.

20Hawa ni wana wa Hamu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.

21Shemu ambaye ni ndugu mkubwa wa Yafethi, kwake kulizaliwa wana pia. Shemu alikuwa baba wa wana wote wa Eberi.

22Wana wa Shemu walikuwa: Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.

23Wana wa Aramu walikuwa: Usi, Huli, Getheri na Mesheki.

24Arfaksadi alikuwa baba wa Shela, naye Shela akamzaa Eberi.

25Eberi akapata wana wawili: Mmoja wao aliitwa Pelegi, kwa kuwa wakati wake ndipo dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani.

26Yoktani alikuwa baba wa: Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,

27Hadoramu, Uzali, Dikla,

28Obali, Abimaeli, Sheba,

29Ofiri, Havila na Yobabu. Hawa wote walikuwa wana wa Yoktani.

30Nchi waliyoishi ilienea toka Mesha kuelekea Sefari kwenye nchi ya vilima iliyoko mashariki.

31Hao ndio wana wa Shemu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.

32Hizi ndizo koo za wana wa Noa, kufuatana na vizazi vyao, katika mataifa yao. Kutokana na hawa mataifa yalienea duniani kote baada ya gharika.

chanzo: Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

WEBREATH · 11:11

«He himself gives everyone life and breath and everything else» — Acts 17:25

Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.

WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath